Ratings & Reviews performance provides an overview of what users think of your app. Here are the key metrics to help you identify how your app is rated by users and how successful is your review management strategy.
Intra hukulinda dhidi ya ughushi wa DNS, uvamizi wa kimtandao unaotumiwa kuzuia ufikiaji wa tovuti za habari, mitandao ya kijamii na programu za kutuma na kupokea ujumbe. Intra pia hukulinda dhidi ya programu hasidi na uvamizi unaonuwia kuiba data yako binafsi. Inaweza kutumiwa kwa urahisi na mtu yeyote — unaweza kuiwasha kisha uendelee na shughuli zako. Intra haitapunguza kasi ya muunganisho wako wa intaneti na hakuna kikomo cha matumizi ya data. Ijapokuwa Intra hukulinda dhidi ya ughushi wa DNS, kuna mbinu zingine changamano za uzuiaji na uvamizi ambazo Intra haiwezi kukulinda dhidi yake. Pata maelezo zaidi katika https://getintra.org/. Vipengele • Uwezo wa kufikia kwa njia wazi tovuti na programu zilizozuiwa na ughushi wa DNS • Hakuna vikomo vya matumizi ya data na haitapunguza kasi ya muunganisho wako wa intaneti • Weka maelezo yako yawe ya faragha — Intra haifuatilii programu unazotumia au tovuti unazotembelea • Weka mapendeleo yako kwenye mipangilio ya mtoa huduma wa seva yako ya DNS — tumia wako au uchague miongoni mwa watoa huduma maarufu • Programu huria